Mtu akipata kazi kwanza anauliza *mshahara* shilingi ngapi.? Kama akiambiwa mshahara kidogo kinyume na matarajio yake atafanya kazi kwa muda mfupi kisha kuacha au kuacha kabisa hiyo kazi.
*Ndugu* kumbuka unapopata fursa ya kufanya kazi mahali fulani ni wakati mzuri wa kujifunza.
Watu wengi "target" yao ya kwanza pindi tu wanapopata sehemu ya kufanya kazi ni kupata pesa.
Hili ni kosa kubwa kwa mtu mwenye lengo la kujiajiri baadaye.
Utanakiwa ujue kuwa wakati huo ni mzuri kwako wewe katika kujifunza na kupata ujuzi huo. Unapaswa kujifunza kila kitu kuhusiana na hiyo shughuli nzima inayoendelea hapo mahali pa kazi.
Fanya kazi kwa malengo ya kupata mahalifa, kuna leo na kesho hutokuwepo hapo kazini, unapaswa kujipatia ujuzi huo bure kabisa.
Watu wengi wamefanikiwa kwa kujifunza kutoka mahali walipokuwekuwa kwa waajiri wao. Na baadaye wakaweza kuanzisha miradi yao na kufanikiwa sana.
Uwepo eneo la kazi hakikisha unajifunza kila ' *details* zinazohusiana na kazi hiyo. Usifikirie tu malipo unayostahili kulipwa, fanya malipo hayo kama kitu cha ziada tu. Kuna faida ya kujifunza, imejificha na wengi hawaioni.
Tafuta kujua kila kitu ujipatie maarifa na jinsi ya kufanya kazi mbali mbali katika eneo lako la kazi au taasisi uliyopo.
Fahamu jinsi ya kuandaa, miradi, jinsi ya kutafuta wahisani, jinsi ya kuandika *proposal* , ripoti, au kama sehemu unayofanya kazi ni ya biashara, fahamu mali ghafi mnatoa wapi, bidhaa mnaandaa jinsi gani, soko huwa mnapataje, mzigo huwa mnausambaza vipi, mnashirikiana vipi na wabia au wadau, changamoto ni zipi, jinsi gani ya kutatua hizo changamoto na faida hupatikana kiasi gani.
Maarifa Kama hayo ni muhimu kuwa nayo.
Ukiwa tayari kujifunza utajipatia ujuzi na utaalamu mkubwa sana. Na hapo ndipo unapojijengea msingi wa kujiajiri hapo baadaye.
Kupitia utaalamu utakaoupata siku moja utaweza kuanzisha mradi wako na kujiajiri.
Ukitaka kujifunza fursa zipo. Siyo lazima uwe katika ajira. Kama huna ajira mtafute mtu anayefanya kitu unachotamani kukifanya. Jitolee kumsaidia kwa moyo mweupe bila hata kutaka malipo. Lakini lengo lako liwe kujifunza kile anachokifanya.
Watu wengi sana wamejifunza kwa njia hii. Nenda kashinde na watu wa gereji utakuwa fundi gereji, nenda kashinde na mfanya biashara nawe utajua biashara, tumia muda wako mwingi kuwa na watu ambao hufanya shughuli ambayo na wewe katika ndoto zako unatamani kufanya shughuli hiyo.
*Swaleh* *Hassan* *Kassu* .
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments: