π Chakula Chenye Wanga
☑️Chakula chenye wanga hupatikana zaidi kutoka kwenye nafaka, mboga, maziwa ya mgando na matunda .
☑️Mwili wa binadamu huhitaji chakula chenye wanga, hatuwezi kuishi bila chakula cha aina hii. ☑️Mwili hubadilisha wanga na kuwa glucose -
☑️aina ya sukari ambayo hutumiwa na seli za mwili kwa ajili ya kupata nguvu na kukua.
☑️Imeonekana kuwa mtu akila kiasi kile kile cha chakula chenye wanga na muda ule ule kila siku.
☑️anakuwa na nafasi kubwa sana ya kudhibiti kiwango chake cha sukari katika mwili.
☑️Ni muhimu kuhakikisha kuwa mgonjwa haruki mlo wo wote kwani kufanya hivyo kutasababisha badiliko kubwa la kiwango cha sukari katika damu yake kitu ambacho kinatakiwa kikwepwe kwa mgonjwa wa kisukari.
☑️Kuwa na ongezeko la glucose katika damu ambalo ni la kawaida kunasaidia kuweza kujua namna ya kuweka uwiano kati ya chakula, dawa na mazaoezi ya mwili na hivyo kudhibiti kiwango cha sukari katika mwili wa mgonjwa.
☑️Uwiano mzuri wa chakula…
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments: