Β» Β» KAYA NA FAMILIA

*NYAMONGO NET-EVENT 2021-AMANI ITOKAYO JUU.*

Jumanne, 21/09/2021.

MCH. BEATUS MLOZI.

*SOMO: MIGOGORO KATIKA NDOA/FAMILIA.*

Migogoro huja baada ya watu kutofautiana kimawazo yaani mpishano wa hoja baina ya mtu na mtu au watu na watu.

Mwanzo 24-27 utakuta mgogoro kati ya Isaka na Rebeka, na Raheli na Lea juu ya watoto.

Lakini Sulemani yeye je anasemaje?

Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi. 
Mithali 17:1

Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.
Mithali 25:24

Migogoro haiepukiki katika maisha hata hivyo ni Mungu ndiye anayetuwezesha kuishinda. Kwamwe usikimbie ndoa yako kwa sababu ya migogoro.

Hata hivyo migogo ina faida na inaleta changamoto chanya maishani.

Aina za migogoto katika familia.

1. Migogoro inayosababishwa na sababu za ndani yaani wanandoa wenyewe.

2. Migogoro ya wapambe(watu wa nje) kutoka nje.

Migogoro kutoka nje husababishwa na watu wafuatao:

1. Mama mkwe, mama wa Bwana arusi. Anaweza kumwambia kijana amwache binti wa kijana wake lakini hawezi kumwambia binti yake kuachika kwa kijana fulani. Hivyo akina amama acheni kuwadanganya watoto wenu mke wa kijana wako ni ni binti yako pia.

2. Mawifi pia ni vyanzo vya migogoro katika ndoa za kaka zao. Ni wasumbufu sana katika ndoa na chanzo cha migogoro.

3. Mama wa bibi arusi naye ana shida. Unasikia akimwambia binti huyo mume akikusumbua rudi nyumbani hujaua. Umeharibu wewe mama mzazi.

4. Mashemeji pia ni shida.

5. Mdogo wa bibi arusi wa kike. Hawa nao ni chanzo cha migogoro. 

6. Baba mkwe. Huyu pia ni chanzo cha mgogoro nyumbani.

*MUNGU ATUSAIDIE SOTE.*
πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called Gsn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
Β«
Next
MACHINGA NI VIJANA WETU" - KATIBU MKUU UVCCM CDE. LULANDALA
Β»
Previous
HISTORIA YA WILAYA YA NGARA, ASILI YA MAJINA MBALIMBALI, UTAMADUNI WA WAKAZI WA NGARA NA CHANZO CHA JINA LA KABILA LA WAHANGAZA WANAOKAA WILAYANI NGARA

π—‘π—π—œπ—” π—”π—¦π—œπ—Ÿπ—œ 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—­π—¨π—œπ—” 𝗑𝗔 π—žπ—¨π—¦π—¨π—žπ—”π—₯π—œ

πŸ“ Chakula Chenye Wanga  β˜‘οΈChakula chenye wanga hupatikana zaidi kutoka kwenye nafaka, mboga, maziwa ya mgando na matunda . β˜‘οΈMw...